Skip to main content
Skip to main content

DCP yatishia kwenda mahakamani kusitisha ukataji miti Aberdare

  • | Citizen TV
    992 views
    Duration: 1:21
    Chama cha DCP kimetishia kuelekea mahakamani kusitisha ukataji miti katika msitu wa Aberdare iwapo Huduma ya Misitu nchini (KFS) haitafichua mpangilio unaofuatwa katika zoezi la kuondoa miti mikuu msituni humo. Wakizungumza katika eneo la Lari, kaunti ya Kiambu, walikohudhuria ibada ya Jumapili, wanasiasa wa DCP wamekosoa zoezi hilo, wakidai linafanywa bila ushirikishwaji wa umma. Aidha, wamedai kuwa upungufu wa maziwa nchini umetokana na mpango wa kubinafsisha Kiwanda cha Maziwa cha KCC, ambao unatarajiwa kuanza mwezi huu.