- 12,465 viewsDuration: 3:15Makamu mpya wa rais wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amechukua rasmi wadhifa huo baada ya kuapishwa leo katika hafla iliyoshuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma. Uapisho huo unajiri huku shinikizo la kufanikisha kupatikana kwa Katiba mpya ifikapo mwaka 2028 likiongezeka. Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Joseph Warioba, ameonya kuwa uchaguzi ujao huenda ukakumbwa na ghasia iwapo mageuzi ya sheria za uchaguzi hayatafanyika.