- 838 viewsDuration: 2:55Mamlaka ya Afya ya Kidijitali - DHA- imetetea ada ya asilimia mbili inayokatwa kutoka kwa madai yanayochakatwa kupitia Mamlaka ya SHA. Mamlaka hiyo inasisitiza kuwa ada hiyo ni halali na inalipiwa kwa huduma zinazotolewa kwa vituo vya afya. Afisa Mkuu wa Mamlaka hiyo Anthony Lenaiyara, amekanusha madai kwamba fedha hizo hulipwa kwa taasisi binafsi, akisema fedha hizo huenda mara hiyo hiyo kwa DHA.