Skip to main content
Skip to main content

Dkt. Belio Kipsang asema vitambulisho vitaanza kutolewa shule za upili

  • | Citizen TV
    2,909 views
    Duration: 1:46
    Katibu wa idara ya uhamiaji na huduma za wananchi Dkt. Belio Kipsang aliongoza zoezi la kuwahamasisha machifu kuhusu mwongozo mpya wa kuwasajili wakenya ambao wamefikisha umri wa miaka 18 ili waweze kupata vitambulisho vya kitaifa. Zoezi hilo ambalo limefanywa katika kaunti 20 sasa kuanzia mwezi Julai mwaka jana limewezesha wizara hiyo kuwasajili watu milioni 1.7 kufikia sasa. Akizungumza katika kaunti ya Bomet, Kipsang, alisema kuwa wanaojiandikisha watapata vitambulisho katika chini ya wiki moja. Hata hivyo mpango huo unalenga kuanzisha usajili kwa shule za upili nchini kuanzia mwezi ujao.