Skip to main content
Skip to main content

Utata kwenye mazungumzo ya Ukraine na Urusi. Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    20,926 views
    Duration: 28:15
    Siku ya pili ya mazungumzo ya kujaribu kumaliza vita nchini Ukraine, yaliyofanyika Abu Dhabi, imekamilika. Urusi na Ukraine zilishiriki katika mazungumzo hayo, huku wajumbe wa Rais Donald Trump, Jared Kushner na Steve Witkoff, wakiyasimamia. Hii ilikuwa duru ya kwanza ya mazungumzo yaliyoandaliwa na Marekani katika kipindi cha miezi tisa baada ya mikutano ya awali kutozaa matunda. Tangazo pekee la wazi lililotolewa ni makubaliano kati ya Urusi na Ukraine ya kubadilishana wafungwa kwa idadi kubwa, hatua ambayo ni ya hivi karibuni katika mfululizo mrefu wa ubadilishanaji wa aina hiyo. Bado kuna tofauti kubwa kuhusu masharti ya kusitisha mapigano, maeneo yanayozozaniwa, na mipango ya usalama ya baadaye barani Ulaya. #putin #zelensky #abudhabi #trump #bbcswahili #tiktok #cop31 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw