Skip to main content
Skip to main content

DRC na M23 wataheshimu usitishaji mpya wa mapigano? Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    15,084 views
    Duration: 28:10
    Pendekezo la usitishaji mapigano lililoratibiwa na Angola kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda linatarajiwa kuanza kutekelezwa leo Jumatano katika eneo la mashariki mwa DRC lililokumbwa na mzozo. Angola, ambayo kwa muda mrefu imekuwa mpatanishi kati ya Rwanda na Congo, inazihimiza pande zote kuheshimu makubaliano hayo ya kusitisha mapigano. Siku ya Ijumaa, serikali ya Congo na waasi wa M23 walikubali kuheshimu usitishaji mapigano uliotangazwa na Rais João Lourenço wa Angola mapema wiki hii. Hata hivyo, hakuna upande uliothibitishia BBC kwamba mapigano yamesitishwa moja kwa moja kwenye uwanja wa vita. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw