- 1,374 viewsDuration: 2:41Katibu wa Idara ya Uhamiaji Belio Kipsang, Naibu Kinara wa Jubilee Dkt. Fred Matiang’i na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi Muhammad Swazuri ni miongoni mwa watu 22 na kampuni tatu zinazolengwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kurejesha mabilioni ya fedha yaliyolipwa kwa marehemu mfanyabiashara Francis Mburu kama fidia ya ardhi ya Ruaraka. EACC imewataka kurejesha fedha hizo ndani ya siku saba kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufaa mwezi jana uliobaini kuwa malipo hayo yalikuwa kinyume na sheria. Gatete Njoroge ana kina cha taarifa hiyo.