Skip to main content
Skip to main content

Emerging Stars kuanza kampeni ya kufuzu AFCON U23

  • | Citizen TV
    876 views
    Duration: 45s
    Timu ya Emerging Stars itaanza kampeni yao ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa chini ya miaka 23, AFCON 2027, Jumatatu, watakapoikaribisha Tanzania mkondo wa kwanza wa raundi ya awali, uwanjani Nyayo. Kikosi hicho chini ya kocha Anthony Kimani kimekuwa kambini kikijiandaa kwa mchezo huo wa mkondo wa kwanza, kabla ya kusafiri kwenda Tanzania kwa mchezo wa marudiano. Mshindi wa jumla kati ya Kenya na Tanzania atamenyana na Côte d’Ivoire katika hatua inayofuata ya kufuzu. Michuano hiyo pia itakuwa sehemu ya mchakato wa kufuzu kwa michuano ya soka ya wanaume katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028 itakayofanyika Los Angeles, Marekani.