- 1,558 viewsDuration: 3:38Kadri nafasi ya kilimo katika maeneo ya mijini inavyoendelea kupungua, wakulima wabunifu wanatafuta mbinu mpya za kuzalisha chakula karibu na makazi yao. Katika kaunti ya Kiambu, familia moja imebadilisha roshani ndogo ya nyumba yao kuwa shamba linalostawi kwa kutumia taa za LED za kukuza mimea. Teknolojia hiyo imewawezesha kuharakisha ukuaji wa mazao mbalimbali licha ya changamoto ya nafasi ndogo na mwanga hafifu wa jua. Mwanahabari wetu Denis Otieno anatuarifu zaidi kwenye Kipindi cha Kilimo Biashara wiki hii.