- 1,005 viewsDuration: 3:15Miezi minane tu baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kihistoria unaopiga marufuku hospitali kuzuia miili, familia moja huko Kigumo imekata tamaa ya kumzika mpendwa wao kutokana na deni la hospitali. Patrick Macharia alilazwa katika Hospitali ya Consolata Mathari kwa miezi 18 kabla ya kufariki. Familia yake imesitisha maandalizi ya mazishi baada ya hospitali kukataa kuachilia mwili hadi familia ilipe deni la shilingi milioni moja.