Familia moja katika eneo la Kibos, kaunti ya Kisumu, inatoa wito wa usaidizi wa kifedha ili kurejesha nyumbani mwili wa jamaa wao aliyefariki dunia nchini Lebanon. Christina Brandy aliondoka Kenya mwaka 2016 kutafuta ajira, lakini juhudi zake zilikatizwa na ugonjwa uliosababisha kifo chake wiki iliyopita. Familia hiyo imesema haiwezi kupata zaidi ya shilingi milioni 1.8 zinazohitajika kurejesha mwili wa Christina nyumbani kwa mazishi na inaomba msaada kutoka kwa serikali na wasamaria wema. Mwanahabari wetu Wycliffe Oketch anatuletea taarifa hiyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive