- 478 viewsDuration: 2:46Familia moja katika kijiji cha sosian, huko Rumuruti kaunti ya Laikipia inalilia haki baada ya mwana wao mwenye umri wa miaka 14 kudaiwa kupigwa risasi na kuuawa na mwenzake wa miaka 15 katika shamba la Ol Donyo Lemora. Kulingana na familia ya marehemu, Peter Edung alipigwa risasi na mwanawe mmiliki wa shamba hilo. Polisi wanasema baba na mwanawe walifikishwa mahakamani ijumaa na kuachiliwa kwa dhamana uchunguzi ukiendelea.