- 8,464 viewsDuration: 3:32Familia ya mfanyabiashara Jimmy Mwanzia Mutava inaishi kwa hofu kufuatia kutoweka kwake katika eneo la Mlolongo, Kaunti ya Machakos. Tukio hilo linajiri kufuatia madai kuwa alitoweka baada ya kukutana na afisa mmoja mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mlolongo. Picha za CCTV zinaonyesha akichukuliwa na watu wanne na kuingizwa kwenye gari. Ode Francis anachambua kanda za CCTV zinazoashiria mara ya mwisho alipoonekana mfanyabiashara huyo.