- 971 viewsDuration: 2:24Familia ya jamaa aliyefariki kufuatia shambulio la msafara wa Linda Mwananchi huko Keumbu, kaunti ya Kisii, inaendelea kusubiri haki. Haya ni huku Mbunge wa Nyaribari Chache, Zaheer Jhanda, ambaye alihitajika kuandikisha taarifa kwa DCI kuhusiana na tukio hilo, sasa akisema kuwa hakuhusika kwa vyovyote vile na kuwa wakazi walilazimika kujilinda baada ya wahuni anaodai walikuwa wameandamana na msafara wa Linda Mwananchi kuwavamia. Willy Lusige anaarifu zaidi.