Familia moja katika eneo la Namanga, kaunti ya Kajiado, imekuwa ikiishi kwa uchungu na maumivu kwa takriban muongo mmoja baada ya jamaa yao kutoweka nchini Afrika Kusini alikokwenda kutafuta kazi. Silas Kipkorir Butia aliondoka humu nchini mwaka wa 2017 kwenda Afrika Kusini kutafuta kazi ya kuwa dereva wa lori, lakini tangu wakati huo familia yake haijapata habari yoyote kuhusu mahali aliko. Juhudi za familia hiyo pamoja na mamlaka husika za kumtafuta hazijazaa matunda. Sasa familia hiyo inatoa wito kwa serikali iwasaidie kumpata jamaa yao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive