- 1,261 viewsDuration: 2:05Familia moja kutoka Nanyuki sasa inadai haki baada ya jamaa yao kupigwa risasi Jumanne wakati wa maandamano ya kupinga ujezi wa kituo cha karantini cha ebola. Sylvester Muigai, mwenye miaka kumi na saba alipigwa risasi kichwani alipokuwa akishiriki maandamano hayo. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, familia hiyo imewalaumu polisi kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi, huku idadi ya vifo vya maandamano hayo ikifikia watu watatu.