Skip to main content
Skip to main content

Familia yadai haki baada ya kijana kuuawa kwa kuchomwa kisu

  • | Citizen TV
    2,967 views
    Duration: 1:26
    Familia moja inadai haki baada ya kijana wao wa miaka 30 kuuawa kwa kuchomwa kisu kufuatia mzozo barabarani karibu na Uwanja wa Nyayo, hapa jijini Nairobi. Marehemu, Kennedy Ng'eno, anadaiwa kushambuliwa na dereva wa teksi baada ya mabishano makali kuzuka kufuatia ajali ndogo ya barabarani. Polisi wanasema mshukiwa alichukua kisu kutoka kwenye gari lake na kumdunga Kennedy kabla ya kutoroka. Maafisa wa DCI wanachunguza kisa hicho kilichotokea saa kumi na moja asubuhi ya Jumamosi.