- 3,235 viewsDuration: 2:23Familia moja katika eneo la Kiminini, kaunti ya Trans Nzoia, imeitaka polisi kumchukulia hatua mwalimu anayetuhumiwa kumpiga mwanafunzi wa kike viboko 30 na kumjeruhi vibaya katika Shule ya Upili ya Masaba. Familia hiyo inasema ni zaidi ya miezi miwili tangu tukio hilo litokee, lakini hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya mwalimu huyo. Aidha, mwanafunzi huyo hajarejea shuleni kwa hofu ya kuadhibiwa zaidi.