- 572 viewsDuration: 3:21Idara ya Polisi imetoa hakikisho kwa familia za waathiriwa wa maandamano ya Juni 25 kuwa watapewa ulinzi wakati wa maandamano ya kumbukumbu yatakayofanyika katika kaunti zote 47. Familia za waathiriwa zilizowasilisha notisi ya kufanya maadhimisho kwa ofisi ya Inspekta Jenerali Douglas Kanja zimetaka kuchukuliwa hatua kwa polisi waliohusika na mauaji, siku hiyo kutangazwa kuwa likizo rasmi na serikali kuomba msamaha kwa maovu yaliyoshuhudiwa.