- 4,524 viewsDuration: 2:41Biwi la simanzi limetanda katika maeneo ya Gilgil na Lanet, kaunti ya Nakuru, huku familia za waathiriwa wa mkasa wa moto katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Utumishi zikiendelea kuomboleza vifo vya ghafla vya wana wao walioteketea usiku wa Jumatano wiki hii. Wakati huo huo, baadhi ya manusura wa mkasa huo wameeleza jinsi walivyopitia wakati mgumu wakijaribu kujiokoa kutoka kwenye bweni lililokuwa likiteketea kwa moto. Mwanahabari wetu Maryanne Nyambura anaripoti kuhusu majonzi yaliyotanda katika familia zilizoathirika na simulizi za manusura kuhusu usiku huo wa kutisha.