Skip to main content
Skip to main content

Familia zaidi ya 200 za Loboi zaishi kwa hofu ya mafuriko

  • | Citizen TV
    436 views
    Duration: 2:23
    Huku taifa likijiandaa kwa mvua kubwa kuanzia mwezi Septemba, zaidi ya familia mia mbili katika kijiji cha Loboi, Kaunti ya Baringo, zinaishi kwa hofu zaidi baada ya kuhamishwa kutokana na mafuriko. Familia hizo ziliathirika na ongezeko la viwango vya maji katika Ziwa Baringo, ambapo maelfu ya ekari za mashamba yameendelea kusombwa kwa zaidi ya muongo mmoja sasa. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, maafisa kutoka serikali kuu walifanya kikao na wakazi kujadili ujenzi wa vizuizi vya maji ili kuzuia hasara na maafa.