- 2,676 viewsDuration: 3:23Familia za vijana watatu wanaodaiwa kutekwa na maafisa wa usalama katika maeneo ya Mathare na Kiamaiko zimetoa makataa kwa serikali kuwaachilia wana wao ndani ya saa 24, la sivyo zitaandamana Jumanne. Familia ya mwanaharakati Davis Lichuma imesema kuwa aliondoka nyumbani kushiriki maandamano ya ukumbusho wa Gen Z kabla ya kudaiwa kuchukuliwa katikati ya jiji na watu wanaoshukiwa kuwa maafisa wa usalama. Familia nyingine mbili pia zimetaka majibu kuhusu kutoweka kwa vijana wao huku zikitaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha wanapatikana salama.