- 3,410 viewsDuration: 3:38Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anadai kuwa kuna njama ya kuingilia shughuli ya usajili wa wapiga kura kwa kuchelewesha utoaji wa vitambulisho kwenye ngome za upinzani. Gachagua sasa akitishia maandamano endapo swala hili halitashughulikiwa. Akizungumza hapa Nairobi, Gachagua pia amesema upinzaniutafanya kikao hapo kesho kutoa muongozo wa maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini.