- 6,440 viewsDuration: 4:03Kinara wa DCP Rigathi Gachagua amejitetea dhidi ya madai ya kukosa kufika kwenye maandamano ya kumbukumbu ya Juni 25, akisema kuwa uwepo wake ungezua vurugu kutokana na madai ya kuandamwa. Akizungumza nyumbani kwake Wamunyoro, Gachagua amesema kutoshiriki kwake kwenye maandamano hayo kulisaidia kuzuia uharibifu wa mali na vurugu ambazo anadai serikali ilipanga kutekeleza na baadaye kumtupia lawama yeye pamoja na vijana. Gachagua pia ametishia kuwashawishi Wakenya kususia kulipa kodi iwapo serikali haitasitisha mpango wa mamlaka ya uchukuzi, NTSA, wa kuanza ukaguzi wa magari ya kibinafsi kuanzia mwezi Julai.