- 2,503 viewsDuration: 2:59Kinara wa DCP Rigathi Gachagua ameishtumu idara ya polisi kwa kile anasema ni kutumiwa vibaya kuzua rabsha kwenye uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Kwenye taarifa nyumbani kwake huko Wamunyoro kaunti ya Nyeri, Gachagua pia ameinyooshea kidole cha lawama tume ya uchaguzi nchini IEBC, akiizoma kwa kusalia kimya licha ya msukosuko ulioshuhudiwa wakati wa uchaguzi huo mdogo.