- 2,885 viewsDuration: 2:58Kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, amemtaja Rais William Ruto kuwa mnafiki kutokana na migogoro ya ardhi ya Kedong na Kibiko katika kaunti za Narok na Kajiado. Akizungumza nyumbani kwake Wamunyoro, kaunti ya Nyeri, kwenye mkutano na baadhi ya viongozi wa mashinani kutoka Narok, Gachagua alidai kuwa Rais Ruto anatumia mvutano huo kama chambo cha kisiasa. Gachagua pia ameahidi kutoa suluhu kwa migogoro ya ardhi katika maeneo ya Kedong na Kibiko.