- 8,867 viewsDuration: 2:05Kinara wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, amemuonya Rais William Ruto dhidi ya jaribio la kumshawishi kinara mwenza wa Wiper, Kalonzo Musyoka, kujiunga naye serikalini kwa ahadi ya kumteua kuwa Naibu Rais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Akizungumza nyumbani kwake Nyeri, Gachagua amemtaka Rais kukoma kujaribu kugawanya upinzani, akidai kuwa ahadi kama hizo zimetolewa pia kwa viongozi wengine katika jitihada za kujinadi kisiasa kwenye ngome tofauti.