Skip to main content
Skip to main content

Gachagua apinga bajeti ya ziada, ataja matumizi ya kisiasa

  • | Citizen TV
    2,317 views
    Duration: 1:25
    Kinara wa DCP Rigathi Gachagua ameendelea kupinga bajeti ya ziada akidai kuna njama fiche katika mgao wa fedha ulioelekezwa Ikulu, Ofisi ya Naibu wa Rais, Wizara ya Usalama na Idara ya Ujasusi (National Intelligence Service Kenya). Gachagua anadai fedha hizo zitatumika kisiasa hususan katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Akiukosoa mgao huo, amesema hauna mantiki kutokana na siku chache zilizobaki kabla ya mwaka wa fedha kuhitimishwa ilhali taifa lina mahitaji mengine muhimu ambayo fedha hizo zingegharamia.