- 4,443 viewsDuration: 1:27Kinara wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua amesema kwamba kinara yeyote wa vyama husika vya Umoja Wa Upinzani atakaye ondoka kutoka kwa mrengo huo basi atakuwa adui wa wakenya. Akizungumza nchini Marekani, naibu rais huyo wa zamani amesisitiza kwamba muungano wa Umoja wa Upinzani utateua mgombea urais mmoja miongoni mwa vinara wa vyama husika kwa lengo la kumtimua rais William Ruto mamlakani kupitia uchaguzi mkuu ujao.