- 668 viewsDuration: 1:26Gavana wa KAUNTI YA KIRINYAGA Anne Waiguru amewakosoa viongozi wa upinzani kutoka eneo la Mlima Kenya kwa madai ya kuibua masuala nyeti ya uongozi ili kujinufaisha kisiasa. Waiguru amesema kujiondoa kwa gavana wa Murang'a Irungu Kang'ata ndani ya chama cha UDA hakutayumbisha ushawishi wa chama hicho katika eneo la Mlima Kenya. Kulingana naye, ataendelea kuunga mkono serikali ya William Ruto ili kuhakikisha ajenda ya maendeleo katika Kaunti ya Kirinyaga na eneo lote la Mlima Kenya inatekelezwa.