Skip to main content
Skip to main content

Gor Mahia yaanza vibaya kampeni za CAF Champions League

  • | Citizen TV
    394 views
    Duration: 1:19
    Mabingwa mara 22 wa Ligi Kuu ya Soka nchini, Gor Mahia, wameanza vibaya kampeni za CAF Champions League baada ya kulazwa mabao 2-0 na Pyramids ya Misri ugani Nyayo, Nairobi. Walid El Karti na Mahmoud Saber waliifungia Pyramids mabao hayo katika dakika ya tano na ya 45 ya kipindi cha kwanza. Mechi ya mkondo wa pili itachezwa Septemba 13 jijini Cairo, huku Gor Mahia ikihitaji ushindi wa mabao matatu bila kufungwa ili kusonga mbele.