- 2,729 viewsDuration: 1:37Klabu ya Gor Mahia imewasilisha kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF pamoja na kombe la ODM@20 kwa familia ya marehemu Raila Odinga katika makazi yake ya Karen, Nairobi. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amesema timu hiyo imetimiza matakwa ya Raila ya kushinda mataji hayo mawili aliyowaagiza kabla ya kuelekea India alikofariki dunia. Mjane wa Raila, Ida Odinga, pamoja na mwana wao Raila Odinga Junior wameahidi kuendelea kuisaidia timu hiyo katika harakati zake za kutafuta mafanikio zaidi siku zijazo. Kogalo walituzwa mataji hayo licha ya kupoteza kwa bao moja bila dhidi ya Nairobi United.