Skip to main content
Skip to main content

Hakimu wa Kangema asimamishwa kazi baada ya kukamatwa na EACC

  • | Citizen TV
    4,746 views
    Duration: 3:14
    Tume ya Huduma za Mahakama imemsimamisha kazi kwa muda hakimu mwandamizi wa Mahakama ya Kangema, Martin Kinyua. Hii ni baada ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kumkamata kwa tuhuma za kuitisha na kupokea hongo. Kwa mujibu wa EACC, hakimu Kinyua na afisa mwanagenzi wa Idara ya Mahakama, Julius Njogu, walipokea rushwa ya shilingi laki moja na elfu sabini kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa Murang'a ili kubadili hukumu dhidi yake baada ya kupatikana na kosa la ulaghai. EACC imesema inawachunguza maafisa wengine wa Idara ya Mahakama kufuatia kuongezeka kwa tetesi za ufisadi miongoni mwa maafisa hao.