- 1,380 viewsDuration: 1:35Timu ya taifa ya soka kwa wanawake Harambee Starlets imekamilisha maandalizi yake tayari kwa mkondo wa pili wa mechi ya kuwania kufuzu michezo ya Olimpiki 2028. Starlets iliinyeshea Ushelisheli mvua ya mabao kumi na moja kwa bila kwenye mechi iliyochezwa Alhamisi uwanjani Ulinzi. Mkondo huo wa pili utachezwa katika uwanja huo Jumatatu huku mshindi wa jumla akichuana na mshindi kati ya Zimbabwe na Malawi katika raundi ya tatu. Kocha Godfrey Oduor anatarajiwa kubadilisha kikosi chake baada ya kujumlisha wanaochezea soka yao nchini pekee kwenye mkondo wa kwanza.