- 425 viewsDuration: 1:52Shughuli ya siku tatu ya kuwatafuta wachimba mgodi waliokwama baada ya mgodi wa Ogago kuporomoma huko Bondo hatimaye imekamilika. Hii ni baada ya maiti za wachimba migodi watatu waliofariki kupatikana.. Kulikuwa na majonzi na huzuni tele familia na jamaa za waliofariki walipokusanyika kwa maombi maalum kuwakumbuka wapendwa wao. Maiti ya mwisho iliopatikana ilikuwa wa mtu mmoja ambaye alimpoteza ndugu yake katika mkasa huu..Familia zikiwataja watatu hao kama watu waliokuwa na bidii kazini. Familia hizi sasa zinaomba serikali na wasamaria wema kuwasaidia na gharama ya mazishi..Kilichosababisha mgodi huo kuporomoka bado hakijtambuliwa..