- 4,334 viewsDuration: 3:38Hofu imeendelea kuwagubika raia wa kigeni kufuatia amri ya serikali kuwataka kuhalalisha uwepo wao nchini, licha ya serikali kuongeza muda wa miezi mitatu wa kuwa na stakabadhi na vibali vya kufanya biashara. Taharruki hiyo imewafikia pia wakimbizi na raia wa kigeni wanaotafuta hifadhi humu nchini na ambao wamepewa vyeti na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi (UNHCR). Wakimbizi hao sasa wanakimbilia ofisi za UNHCR jijini Nairobi kutafuta hifadhi.