1,621 views
Duration: 8:24
Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza bado yapo na hayajavunjwa. Hii ni kufuatia ghasia zilizoibuka wikendi hii ambapo Israel na Hamas walishutumiana kwa kuvunja mkataba huo. Israel imesema imeanza “utekelezaji upya” wa usitishaji wa mapigano baada ya kufanya mashambulizi ya anga yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu arobaini, kwa mujibu wa maafisa wa afya huko Gaza. Israel pia imeituhumu Hamas kwa kuwaua wanajeshi wawili wa Israel karibu na mji wa Rafah kusini mwa Gaza, madai ambayo Hamas imeyakanusha.
#Gaza #Israel #Trump
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw