- 4,588 viewsDuration: 2:30Idadi ya makundi ya wahalifu na magenge hatari nchini imeongezeka na kufikia 109. Kulingana na ripoti ya Wizara ya Usalama, maeneo ya Magharibi, Bonde la Ufa na Nairobi yana idadi kubwa zaidi ya magenge hayo nchini. Serikali imesema inalenga kukabiliana na shughuli za magenge hayo, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa vijana kutumiwa kuchochea ghasia za kisiasa.