- 1,716 viewsDuration: 2:39Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imepata pigo mara mbili baada ya Bodi ya Uthibiti wa Ununuzi wa Bidhaa za Umma kuiagiza kurekebisha na kutangaza upya zabuni ya teknolojia itakayotumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, kutokana na ukosefu wa uwazi. Bodi hiyo pia imeitaka IEBC kufanya marekebisho katika zabuni nyingine ya karatasi za kupigia kura, baada ya walalamishi wawili kuwasilisha malalamishi mbele ya bodi hiyo.