- 474 viewsDuration: 2:22Tume ya Uchaguzi, IEBC, imetoa mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa kampeni za uchaguzi mkuu ujao. Kulingana na tume hiyo, mgombea wa urais hataruhusiwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 4.4 katika kampeni. Aidha, maeneo yenye ukubwa mkubwa wa kijiografia, kama kaunti za Marsabit, Wajir na Turkana, yatapewa viwango vya juu zaidi vya matumizi ya kampeni kutokana na ukubwa wake. Mwandishi wetu wa masuala ya siasa, Stephen Letoo, anaangazia kwa undani mapendekezo hayo.