- 2,301 viewsDuration: 3:07Mamlaka ya Kuangazia Utendakazi wa Polisi (IPOA) imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano yaliyoshuhudiwa katika mitaa ya Mathare na Huruma kwa siku tatu. Hatua hii inajiri huku idadi ya waliofariki kufuatia maandamano hayo ikifikia watu watatu. Wakati huo huo, wafanyabiashara wamekadiria hasara kubwa kufuatia uharibifu wa mali uliojitokeza wakati wa vurugu hizo, kama Franklin Wallah anavyotuarifu.