Skip to main content
Skip to main content

IPOA yalalamikia kucheleweshwa kwa uchunguzi wa kifo cha Rex Masai

  • | Citizen TV
    1,210 views
    Duration: 2:58
    Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi (IPOA) imelalamikia kuhangaishwa na maafisa wa polisi katika kesi inayoendelea ya kubaini aliyemuua Rex Masai wakati wa maandamano ya Juni 20, 2024. Wakizungumza mahakamani leo, mawakili wa IPOA walisema hakuna afisa hata mmoja wa polisi kutoka vituo vya Bunge, KICC, Kamukunji na Kilimani aliyeandikisha taarifa kuhusu kesi hiyo. Hata hivyo, mawakili wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi wamesema baadhi ya maafisa hao walihamishwa.