- 1,132 viewsDuration: 3:23Jamaa za waathiriwa wa maandamano ya Gen Z kwa mara ya kwanza walipata fursa ya kuweka mashada ya maua nje ya majengo ya Bunge tangu wana wao walipouawa miaka miwili iliyopita. Licha ya kutatizwa kwa muda, jamaa hao walifanikiwa kutembea hadi eneo la Bunge katika shughuli ya kuwaenzi waliopoteza maisha wakati wa maandamano hayo. Huku wakisisitiza wito wao wa kutaka haki itendeke, familia hizo zinasema bado zinaendelea kusubiri uwajibikaji miaka miwili baadaye.