- 20 viewsBaraza la jamii ya Wabajuni walio wachache katika Kilifi kaunti limetoa wito kwa serikali ya kaunti na serikali ya kitaifa kuhakikisha jamii hiyo inapewa nafasi zaidi za ajira. Viongozi wa jamii wanasema hatua hiyo itasaidia kuimarisha ushirikishwaji, kupunguza ukosefu wa ajira na kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi miongoni mwa wanajamii.