- 311 viewsDuration: 1:38Baraza la jamii ya Wabajuni walio wachache katika kaunti ya Kilifi limetoa wito kwa serikali ya kaunti na serikali ya kitaifa kuhakikisha jamii hiyo inapewa nafasi zaidi za ajira. Viongozi wa jamii hiyo wanasema hatua hiyo itasaidia kuimarisha ushirikishwaji, kupunguza ukosefu wa ajira na kuboresha hali ya maisha ya wanajamii kupitia fursa sawa za kiuchumi.