Skip to main content
Skip to main content

Jamii zashauriwa kuwawezesha wanawake kiuchumi

  • | Citizen TV
    170 views
    Duration: 1:45
    Jamii zimetakiwa kuimarisha juhudi za kuwawezesha wanawake kama njia ya kukuza maendeleo na kukabiliana na changamoto zinazowakumba vijana. Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wanawake wa P.A.G Kenya 2026 uliowakutanisha zaidi ya wanawake 6,000, Mshauri wa rais kuhusu haki za wanawake Harriette Chiggai amesema kuwa wanawake wana nafasi muhimu katika kuanzisha programu za uwezeshaji kupitia vikundi vyao. Mkutano huo wa siku tano pia umelenga kuwaunganisha wanawake na fursa za kiuchumi, mipango ya serikali pamoja na huduma za kijamii huku pia ukiibua wasiwasi kuhusu ongezeko la wajane katika Kaunti ya Vihiga.