- 1,894 viewsDuration: 3:11Familia za wanaume wawili wanaodaiwa kukwama kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka katika mtaa wa South C, Nairobi, zinataka operesheni ya uokoaji kuimarishwa. Familia hizo zilizoshinda eneo hilo tangu mkasa huu ulipotokea mapema hapo jana pia zikitaka uchunguzi wa kina kufanywa kuhusu kuporomoka kwa jengo huli wakisema waliohusika na hatia za ujenzi duni wachukuliwe hatua