- 7,862 viewsDuration: 2:44Waziri wa Madini Hassan Joho amepuzilia mbali madai ya Kinara wa DCP Rigathi Gachagua kwamba anashirikiana na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Fahima Araphat Abdallah kwenye njama ya wizi wa kura. Akizungumza katika Kaunti ya Lamu, Joho amesema madai hayo hayana msingi wowote na kuwa Gachagua anamlenge Fahima kwa kuwa anatoka katika jamii ndogo. Na kama anavyoarifu Gatete Njoroge, Joho amesisitiza kuwa juhudi zake zote ni kuwarai wananchi kumpigia Rais William Ruto kura kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu ujao.