- 578 viewsDuration: 3:08Uchunguzi wa maiti umebaini kuwa marehemu Joseph Kamau kutoka eneo la Majengo katika kaunti ya Nyeri alifariki kutokana na risasi ya kichwa. Kijana huyu alikuwa mmoja wa watu waliofariki wakati wa maandamano dhidi ya ongezeko la bei ya mafuta wiki iliyopita. Na huku familia yake ikililia haki, maelfu ya watu wengine walioathirika na maandamano ya awali bado wanasubiri fidia. Tume ya Haki za Binadamu ya KNCHR imesema kuwa fedha hizo hazijatolewa na serikali.