Skip to main content
Skip to main content

Junior Starlets yaelekea Afrika Kusini kwa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia

  • | Citizen TV
    200 views
    Duration: 49s
    Kikosi cha Junior Starlets kimeondoka kuelekea Afrika Kusini kwa mechi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 dhidi ya wenyeji Bantwana, itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Lucas Moripe mjini Pretoria. Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mildred Cheche kinalenga kufuzu kwa mara ya pili kwenye Kombe la Dunia la Wanawake kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 litakalofanyika Morocco. Junior Starlets iliweka historia mwaka 2024 kwa kuwa timu ya kwanza ya taifa ya Kenya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kushiriki mashindano yaliyofanyika Jamhuri ya Dominika. Baada ya mkondo huo wa kwanza, timu hizo zitarudiana Julai 12 katika Uwanja wa Nyayo, ambapo mshindi wa jumla atafuzu kwa mashindano hayo.